Arusha
Home » » MKURUGENZI MKUU NIDA ATEMBELEA NA KUKAGUA HATUA ZA UJENZI WA OFISI ZA WILAYA MKOANI ARUSHA

MKURUGENZI MKUU NIDA ATEMBELEA NA KUKAGUA HATUA ZA UJENZI WA OFISI ZA WILAYA MKOANI ARUSHA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA Ndg. Andrew W. Massawe akiweka saini kwenye kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Wilaya ya Longido na kupokelewa na Katibu Tawala.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA (kushoto), akifuatiwa na Afisa Usajili Wilaya ya Longido Ndg. Tarimo wakisikiliza taarifa ya mwenendo wa Usajili wananchi kwa Wilaya ya Longodo iliyowasilishwa na Katibu Tawala Ndg. Toba Nguvila (Katikati). K kulia ni Ndugu Alphonce Malibiche Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uzalishaji.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA Ndg. Andrew W. Massawe (wa kwanza kushoto) akiwa ameambatana na Katibu Tawala Wilaya ya Longido Ndg.Toba Nguvila wakiwa wamewasili kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi za NIDA wilaya ya Longido na kupokelewa na mkandarasi wa ujenzi ndugu Kim na maafisa wengine.
  Muonekano wa Ofisi ya Usajili Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Wilaya ya Longido mkoani Arusha, ikiwa katika hatua za mwisho za ujenzi.



Kaimu Mkurugenzi Mkuu (NIDA) Ndg. Andrew W. Massawe ametembelea na kukagua hatua za ujenzi wa majengo ya ofisi katika Mkoa wa Arusha; na kukutana na viongozi mbalimbali wa mkoa huo kujadili maendeleo ya zoezi la Usajili wananchi linaloendelea nchini kote.

Ujenzi wa Ofisi za NIDA unaoendelea katika Wilaya za Arusha, Arumeru na Longido ni mradi wa mkopo wenye masharti nafuu unaofadhiliwa na Serikali ya Korea Kusini.

Akizungumza na Katibu Tawala Wilaya ya Longido mara baada ya kukamilisha ukaguzi wa majengo hayo; ndugu Massawe amesema majengo hayo yatawezesha NIDA kufanikisha malengo ya Usajili kwa asilimia kubwa, pamoja na kurahisisha usafirishaji wa Data kwenda makao makuu ya uzalishaji Vitambulisho kwakuwa majengo hayo yamejengwa kisasa na yana miundombinu ya kuwezesha uzalishaji wenye kukidhi vigezo vinavyohitajika kutokana na teknolojia inayotumika.

Wilaya ya Longido Mkurugenzi huyo alipokelewa na Katibu Tawala Ndg. Toba Nguvila kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo ambaye ameishukuru NIDA kwa hatua kubwa ya ujenzi wa jengo la kisasa kwenye wilaya mpya ya Longido; ambalo si tu litasaidia kuondosha uhaba wa Ofisi lakini kuwezesha Taasisi nyingine kama RITA na Uhamiaji kupata ofisi zitakazowahudumia wananchi kwa ufanisi mkubwa zaidi tofauti na hali ya sasa.

Kwa mujibu wa Mkandarasi Kampuni ya KT –Korea; Ujenzi wa majengo hayo unatazamiwa kumalizika mapema mwezi Mei mwaka huu; na kukabidhiwa NIDA kwa ajili ya kuanza matumizi.


 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa