Arusha
Home » » SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA) SASA LAFIKILIA KUJA NA UTALII KWA BODA BODA NA BAJAJI

SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA) SASA LAFIKILIA KUJA NA UTALII KWA BODA BODA NA BAJAJI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli  ,Juanito Oiarzabal akiwa katika kilele cha Uhuru mara baada ya kufanikiwa kufika huku akiendesha baiskeli . 
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli  ,Juanito Oiarzabal (katikati) akiwa na wenzake wawili ,Eduardo Pascuaz(kushoto)  na Ramon Abecia (Kulia) katika kilele cha Uhuru walipoanda kwa kutumia baiskeli .
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli  ,Juanito Oiarzabal aakiwa na wenzake wawili ,Eduardo Pascuaz na Ramon Abecia walipoianza safari ya kuelekea kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli  ,Juanito Oiarzabal (katikati) akiwa na wenzake wawili ,Eduardo Pascuaz(kushoto)  na Ramon Abecia (Kulia) walipofika katika kituo cha kupumziki cha Horombo.
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli  ,Juanito Oiarzabal akiendesha baiskeli katika eneo la Saddle wakati wa kuekelea kituo cha Kibo .
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli  ,Juanito Oiarzabal akikokota baiskeli yake  katika eneo lenye mawe wakati akiekelea kituo cha Kibo 
Muongoza Watalii,Ally Chuwa akitoa msaada wa kufunga viatu kwa Ramon Abecia wakati akielekea kituo cha Kibo.

Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadi za Taifa ,(TANAPA) Pascal Shelutete akizungumza mara baada ya wageni hao kushuka baada ya kufanikiwa kufika kilele cha uHuru kwa kutumia Baiskeli.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limesema litafikiria matumizi ya Boda boda na Bajaji kwa wageni watakao hitaji kutembelea Hifadhi zake endapo yatajitokeza maombi ya kutosha kuhusu matumizi ya vyombo hivyo.

Hatua hiyo inatokana na bidhaa mpya ya Utalii wa kutumia Baiskeli iliyoanzishwa hivi karibuni katika Hifadhi za Taifa za Mlima Kilimanjaro na Arusha kuanza kuwa kivutio kwa watalii kutoka nchi mbalimbali walioanza kufanya utalii wa Baiskeli.

Miongoni mwa watali hao ni pamoja na mpanda  milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli  ,Juanito Oiarzabal aliyeweka rekodi ya kuwa Mhispania wa kwanza kupanda Mlima Kilimanjaro huku akitumia saa 31 akiendesha baiskeli katika siku tano hadi kufika kilele cha Uhuru.

Juanito na wenzake wawili , Eduardo Pascuaz na Ramon Abecia waliianza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli ,wakianza safari yao kupitia lango la Kilema ,aina hi ya utalii ikiwa ni bidhaa mpya katika Milima huo mrefu kuliko yote barani Afrika.
Aina hii mpya ya utalii ambayo kwa sasa imeanza kushika kasi katika Hifadhi za Taifa ,za Mlima Kilimanjaro,Arusha na Saadan inatokana na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kuendelea kupanua wigo wa vivutio katika Hifadhi zake 16,
Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete amesema hatua ya Juanito na wenzake kufika katika kilele cha Uhuru inaashiria kuanza kufunguka kwa aina hii mpya ya utalii katika Hifadhi za Taifa .
Shelutete amesema namna ambavyo Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) limekuwa mstari wa mbele katika kubuni aina mpya ya bidhaa za utalii ili  kushindana na nchi nyingine duniani katika uuzaji wa safari kwa watalii.
Kwa upande wake Juanito Oiarzabal ambaye amepata ulemavu wa kukatika vidole kutokana na barafu katika Milima mbalimbali aliyopanda amesema changamoto aliyokutana nayowakati wa kupanda mlima ni kuzoea hali ya hewa yam lima ambayo imekuwa ikibadilika kila mara.
Mkurugenzi wa kampuni ya Safari Bike Africa iliyoratibu changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli kwa wageni hao,Mario Martos amesema kampuni yake imekusudia kuleta mabadiliko katika sekta ya utalii kwa kufanikisha safari za watalii wa kutumia baiskeli.
Shirika la Hifdhi za Taifa (TANAPA) limejipanga kuhakikisha usalama wa hali ya juu kwa wageni watakaofanya aina hii mpya ya utalii katika Hifadhi zake kwa kuwa na taahadhari sambamba na waongoza wageni waliobobea katika kazi ya Utalii.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa