Arusha
Home » » RC GAMBO ATIMIZA AHADI ZAKE KWA WANA ARUMERU

RC GAMBO ATIMIZA AHADI ZAKE KWA WANA ARUMERU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 RC Gambo akikabidhi mifuko ya saruji kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha Ndg Charles Mahera (katikati) aliyeambatana na Katibu Tawala wa wilaya ya Arumeru Ndg. Timoth Mzava
 Lori lililosheheni mifuko 700 ya saruji tayari kuelekea makao makuu ya Halmashauri yaArusha
 RC Gambo akikabidhi mabati kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha
RC Gambo akikabidhi nondo tani mbili kwa wananchi wa wilaya ya Arumeru


Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo amekabidhi vifaa vya ujenzi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zake alizotoa katika ziara yake ya siku tano iliyomalizika tarehe 15/09/2017.

Katika makabidhiano hayo Mhe. Gambo amekabidhi jumla ya mifuko 700 ya saruji, nondo za ukubwa wa milimita 16 na 12 tani moja moja na bati 200 kwenda kukamilisha ujenzi wa miundombinu mbalimbali.

Katika ziara yangu nimekutana na wananchi wetu wamejitahidi kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo na Halmashauri ya Arusha Vijijini imefanya kazi kubwa, wakaniomba mimi kama Mkuu wa mkoa niweze kuchochea shughuli za maendeleo……na msaada huu utaenda kusaidia maeneo mbalimbali mfano ujenzi wa daraja Mateves na nyumba za walimu Oldonyosambu”* alisema Mhe. Gambo.

Mkuu wa Mkoa amemaliza ziara zake za kikazi katika mkoa wa Arusha kwa kutembelea Halmashauri 7 na wilaya zote 6, ziara hizi zikiwa na lengo la kujitambulisha kwa wananchi na kusukuma shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa