Arusha
Home » » MKUU WA WILAYA YA MONDULI MHE. IDDI HASSAN KIMANTA AONGOZA MAZISHI YA WATOTO WATATU WALIOFARIKI DUNIA BAADA YA KULIPUKIWA NA BOMU

MKUU WA WILAYA YA MONDULI MHE. IDDI HASSAN KIMANTA AONGOZA MAZISHI YA WATOTO WATATU WALIOFARIKI DUNIA BAADA YA KULIPUKIWA NA BOMU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Wanafunzi wa shule ya msingi Nafcon wakiwa wamebeba majeneza yenye miili ya wanafunzi wenzao mara baada ya kuwasili nyumbani kutokea hospitali ya wilaya ya Monduli kabla ya mazishi katika Kijiji cha Nafco kilichopo Kata ya Loksale wilayani Monduli, Mkoa wa Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Iddi Hassan Kimanta akitoa rambirambi za serikali kwenye mazishi hayo katika Kijiji cha Nafco kilichopo Kata ya Loksale wilayani Monduli, Mkoa wa Arusha baada ya shughuli ya kuaga miili hiyo katika Hospitali ya Wilaya ya Monduli.


Mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe. Iddi Hassan Kimnta akifuatiwa na Brigedia Jenerali Athanasi Mbonye, Kamanda wa Brigedi ya Mbuni, na Brigedia Jenerali R.G. Hanti wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu kabla ya mazishi.


Ibada ya mazishi katika Kijiji cha Nafco kilichopo Kata ya Loksale wilayani Monduli, Mkoa wa Arusha
Sehemu ya waombolezaji kwenye mazishi hayo

Askari wa JWTZ wakiwa wamebeba moja ya majeneza ya marehemu hao wakielekea makaburini kwa mazishi. Picha zote na HD TEAM MEDIA.


Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Iddi Hassan Kimanta leo ameongoza waombolezaji katika mazishi ya watoto watatu waliofariki dunia kwa mlipuko wa bomu kwenye eneo la mazoezi ya kijeshi wilayani Monduli, mkoani Arusha.

Marehemu hao - Johnson Daniel, Lendisi Saitabau na Samweli Nyangusi -walifariki dunia Ijumaa iliyopita katika Kijiji cha Nafco kilichopo Kata ya Loksale walipokuwa wakichunga ng'ombe. Inasemekana walilipukiwa na bomu walipokuwa wakilichezea wakidhani ni mpira.

Mazishi hayo yamefanyika katika Kijiji cha Nafco kilichopo Kata ya Loksale wilayani Monduli, Mkoa wa Arusha baada ya shughuli ya kuaga miili hiyo katika Hospitali ya Wilaya ya Monduli.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa