Arusha
Home » » WAHOJI MADIWANI WALIOJIUZULU

WAHOJI MADIWANI WALIOJIUZULU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


Imeandikwa na Veronica Mheta, Arusha

BAADHI ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Vijijini, wamehoji ni kwa nini madiwani waliojiuzulu nafasi zao wilayani Arumeru, wameajiriwa kwenye halmashauri hiyo, hali inayonyima fursa kwa wananchi wengine wenye sifa na vigezo.
Diwani wa Kata ya Olturoto kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Baraka Simon alihoji kwa nini madiwani hao wafanye kazi wakati walishajiuzulu.
“Ni kwa nini madiwani wa Wilaya ya Meru waliojiuzulu nafasi zao wameajiriwa katika Halmashauri ya Arusha Vijijini na je, hamuoni kuwa wanawanyima wenzao fursa za ajira, hii inashangaza,” alieleza Simon, alipouliza swali la papo kwa papo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya nne ya mwaka 2016/17 cha Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Vijijini.
Akijibu swali hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha Vijijini, Dk Charles Mahera alisema ni kweli madiwani hao wapo katika halmashauri hiyo, wanafanya kazi idara mbalimbali kwa kujitolea hadi hapo serikali itakapotangaza nafasi za ajira mpya.
Alisisitiza kuwa waliomba nafasi za ajira katika idara mbalimbali, hivyo wanasubiri ajira zitangazwe kisha wenye sifa waomba. Pia Diwani wa Viti Maalumu, Lulu Ndosi (Chadema) alihoji ni kwa nini walimu wenye digrii wanafundisha shule za msingi wakati wanastahili kufundisha shule za sekondari.
CHANZO HABARI LEO

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa