Arusha
Home » » WAZIRI MKUU MH. KASSIM MAJALIWA AZUNGUMZA NA WAFANYABIASHARA JIJINI ARUSHA

WAZIRI MKUU MH. KASSIM MAJALIWA AZUNGUMZA NA WAFANYABIASHARA JIJINI ARUSHA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 Mhe.Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa  akizungumza na wafanyabiashara wa Jiji la Arusha katika ukumbi wa AICC,Jijini Arusha.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo(kulia) na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Lekule Laiza(kushoto).


Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Mjaliwa amewata wafanyabiashara kuwekeza zaidi kwenye sekta mbalimbali hasa za viwanda hapa nchini.

Aliyasema hayo alipokutana na wafanyabiashara wa jiji la Arusha nakuwashauri wawekeze kwenye mikoa yote ya Tanzania hasa kwakuanzisha viwanda,ilikujenga nchi ya viwanda kama dhamira ya serikali ilivyo.

“Nawashuri muwekeze kwenye mikoa yote hapa nchini na niruksa kabisa viwanda vingi vianzishwe”.

Hata hivyo amewata waendelee  kushirikiana na serikali yao ya awamu ya tano kwakuwa ipo pamoja nao na inaongeza ulinzi zaidi kwa wafanyakazi wote nchini ili wawe na amani na waweze kuwekeza zaidi.

Serikali ya awamu ya tano itaendelea kuboresha zaidi kwenye sekta binafsi hasa kwakupambana na wasiolipa kodi ili walipe nakuweka usawa katika biashara na kukuza ushindaji wa biashara.

Aidha Majaliwa amewataka watendaji wa serikali kuvilinda viwanda vya ndani kwakuhamasisha matumizi  ya rasilimali za ndani napia kuzipunguzia ushuru ili viwanda viweze kukuwa kwa kasi kama serikali inavyodhamiria kujenga nchi ya viwanda.

Majaliwa bado anaendelea na ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Arusha kwa kutembelea halmashauri zote za Mkoa.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa