MSHITAKIWA EXIM BANK ATAKA AFUTIWE KESI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Imeandikwa na John Mhala, Arusha
MSHITAKIWA wa kwanza katika kesi inayowakabili washitakiwa 15 wakiwemo 13 waliokuwa wafanyakazi wa Benki ya Exim (T) Tawi la Arusha, Bimel Gondael (37), ameiambia mahakama kuwa mashahidi 37 wa jamhuri waliotoa ushahidi katika mahakama hiyo hakuna aliyesema yeye aliharibu nyaraka za benki hiyo.
Gondael ambaye ni Mtanzania mwenye asili ya Kiasia na alikuwa meneja mzoefu katika benki hiyo tangu 2009 hadi 2012, alidai hayo wakati akiongozwa na wakili wake, Adam Jabir mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha/Arumeru, Deusdedit Kamugisha. Gondael ambaye ni shahidi wa 15 wa upande wa utetezi, alidai kutokana na mashahidi wa jamhuri kutomtaja kuhusika na shitaka hilo, aliomba mahakama kumwachia huru.
Alidai Benki ya Exim haikuwahi kutoa taarifa kuwa ilipata hasara kutokana na wizi uliotokea mwaka 2012 na hakuna shahidi wa benki hiyo aliyesimama katika mahakama hiyo kueleza kuwa benki ilipata hasara au Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) nayo ilipata hasara kutokana na wizi huo.
“Lazima kuwe na taarifa ya kifedha ya kila mwaka ya kuonesha hasara na faida na katika kesi hii lazima taarifa hiyo ya ukaguzi wa ndani au nje ingeletwa hapa mahakamani kuthibitisha hilo lakini halikufanyika. Shitaka hili siyo la kweli dhidi yangu na hakuna shahidi aliyethibitisha kuwa niliharibu nyaraka za Benki ya Exim, hivyo naomba mahakama niachie huru,” alidai Gondael.
CHANZO HABARI LEO

VIJANA ZAIDI YA 60 WAMLALAMIKIA MUWEKEZAJI KWA KUWARUDHA FEDHA ZAO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.  wamama wa kijiji cha Sambaru wakiendelea kutwanga mawe kwa ajili ya kuweka tayari kwa kupatikana madini ya  ya zahabu
baadhi ya vijana wa kijiji cha sambaru
Na Woinde Shizza,SingidaZaidi ya vijana 60 wa kijiji cha Sambaru kata ya Ikungi  wilayani Igungi mkoani Singinda wamemlalamikia mwekezaji wa kampuni ya  Sambaru  Gold Mining kwa kitendo cha kuwarusha fedha za malipo  ya kazi walikuwa wakimfanyia mgodini kwake

 Wakiongea na waandishi wa habari kijijini hapo baadhi ya vijana hao walisema kuwa wamefanya kazi katika kampuni hiyo kwa kipindi cha mda mrefu lakini muwekezaji huyo ajawalipa ela zao  na badala yake amewafukuza kazini hapo bila kuwalipa malipo yoyote .Mmoja wa vijana hao aliyejitambulisha kwa jina la Saidi Hassan alisema kuwa walishapeleka malalamiko yao kwa viongozi wa kijiji  lakini hakuna hatua  yeyote iliyochukuliwa hivyo wameiomba serikali iwasaidie ili wapate mafao yao kwani fedha hizo walikuwa wanazitegemea katika kuwasaidia katika majukumu mbalimbali ya kifamilia.“tumekuwa tunamfata muwekezaji huyu na kumuomba  atulipe fedha zetu lakini amekuwa anatukana na kusema atudai ,mbaya zaidi kunawakati alifikia hatua ya kukamata baadhi ya wenzetu ambao wanamdai na kuwapeleka polisi,”alisema SaidiKwa upande wake kijana mungine aliyejitambulisha kwa jina la Fredy John alisema kuwa kunakipindi walishawahi kumpeleka polisi alipofika na kuulizwa kama vijana hao wanamdai alikuabali na akahaidi kuwalipa na aliomba mda na akapewa kimaandishi lakini ,muda huo umepita na hadi leo vijana hao awajalipwa na amefikia hatua ya kuwakana kabisaGazeti hili lilimtafuta mwenyekiti wa kijiji hicho cha Sambaru Mfaume Hassan  ili kubainisha kama anataarifa za vijana hawa nae alisema kuwa ni kweli anataarifa za vijana hawa na alishamtumia mmiliki wa kampuni hiyo taarifa za kuwalipa vijana hawa lakini hajateleza   hivyo ameamua kupeleka swala hili katika ngazi za juu ili  wamsaidie“sisi kama kijiji tumekuwa tuna utaratibu wa  kuwapa vijana wawekezaji hawa nah ii inatokana na uhitaji wa muwekezaji ,unakuta muwekezaji anataka vijana wa kumsaidia kazi uko mgodini kwake analeta barua katika ofisi ya kijiji  na sisi tunampa  vijana na ndio utaratibu uliofanywa sasa muwekezaji huyu kaja kuchukuwa vijana lakini cha kushangaza wamefanya kazi mgodini kwake lakini ajawalipa mpaka leo na mbaya zaidi akifatwa anasema kuwa adaiwi kitu ambacho sio cha kweli mimi kama kiongozi wa kijiji nikishirikiana na wenzangu tutajitaidi kufuata sheria ili vijana hawa walipwe ela zao na hadi sasa navyoongea nilishampa taarifa mkuu wa wilaya”alisem Mwenyekiti wa kijiji Mfaume HassanGazeti hili lilimtafuta  mmiliki wa kampuni ya Sambaru  Gold Mining Ahamed Magoma  kujibu  tuhuma hizi nae alisema kuwa yeye kama yeye adaiwi na kijana yeyote Yule wa kijiji cha Sambaru ,na kama kuna mtu anae mdai afuate  vyombo husika vya sheria akamdai“mimi sidaiwi na kijana yeyote Yule vijana wangu wote ambao nawaajiri  nawalipa vizuri na wengine wapo kazini hadi sasa,pia mimi sijawai kwenda kijijini kutafuta kijana wa kunifanyia kazi na napenda kusema ivi kama kuna mtu ambae ananidai afuate sheria  ,aje na vielelezo anidai  na kama ni kweli nitamlipa ila sidaiwi na mtu yeyote “alisema MagomaAkiongelea swala hilo mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu alisema kuwa swala hilo alishalipokea kutoka kwa mwenyekiti wa kijiji cha Sambaru  na alimuagiza aandike idadi ya vijana hao pamoja na majina yao ili ayafanyie kazi ,aidha pia alisema kuwa atamuandikia barua  ya kumuita ofisini kwake  mmiliki wa mgodi huo wa Sambaru Gold Mining .

video


CHUO CHA UFUNDI ARUSHA CHAZINDUA MTAALA MPYA WA GESI NA MAFUTA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Hagnery Chitukulo akizungumza wakati wa ufunguzi wa kozi ya ufundi bomba,mafuta na gesi katika chuo cha Ufundi Arusha(ATC) jijini Arusha,kushoto ni Mkuu wa Chuo cha  Camosun nchini Canada,Sherri Bell na kulia ni Mkuu wa Chuo cha ATC,Dk Richard Masika.

Afisa wa kitengo cha biashara katika ubalozi wa Canada nchini,Anita Kundy akisoma hotuba yake,kushoto ni Mshauri wa ufundi kutoka nchini Canada,Dk Alan Copeland.

Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Hagnery Chitukulo akionesha nakala ya mtaala mpya wa  kozi ya ufundi bomba,mafuta na gesi uliozinduliwa katika chuo cha Ufundi Arusha(ATC)

Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi nchini(TVET)Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Mhandisi Thomas Katebalirwe akizungumza jambo katika hafla ya uzinduzi huo.


Baadhi ya wanafunzi wa mwanzo wa kozi ya ufundi bomba na utaalamu wa gesi na mafuta katika Chuo cha ufundi Arusha

Mgeni rasmi Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Hagnery Chitukulo(wa tatu kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na wageni kutoka Chuo cha Camosun,Victoria nchini Canada na Chuo cha ATC.Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Hagnery Chitukulo amekipongeza Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) kwa uamuzi wake wa kushirikiana na Chuo cha Camosun cha nchini Canada kuandaa mtaala wa ufundi bomba,gesi na mafuta katika ngazi ya Diploma.

Akizindua mtaala huo ambao ni kwanza na aina yake nchini alisema utaisadia serikali kuwapata vijana wengi wenye utaalamu wa sekta ya mafuta na gesi nchini katika ngazi hiyo ambayo imenekana kuna pengo kubwa nchini.

"Mafunzo haya yatasaidia sana kuwapata wataalamu wetu na itaipunguzia serikali mzigo wa kuwaajili wataalamu wa kigeni ambao ulipwa fedha nyingi za kigeni,"alisema

Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha,Dk Richard Masika amesema baada ya kutambua mahitaji makubwa ya wataalamu wa fani hiyo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita walikua wakiaanda mtaala kwa ushirikiano na Chuo cha Camosun na mafanikio yamepatikana.

Alisema kozi hiyo ni nyumbufu itakayowawezesha wanafunzi kufanya kazi baada ya kumaliza mwaka wa kwanza na baadaye kuendelea na masomo jambo ambalo litakua likiwapa maarifa kwa vitendo zaidi badala ya nadharia pekee.

Mmoja wa wanafunzi wanaosoma kozi hiyo ambayo imegharamiwa na serikali ya Tanzania,Latifa Mkombo amesema wanaishukuru serikali kwa kutoa ufadhili huo na kuahidi kusoma kwa bidii kwaajili kuingia katika ajira za gesi na mafuta.

WAZIRI MHAGAMA AZITAKA HIFADHI ZA TAIFA KUTUMIA WASANII KATIKA KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
WAZIRI wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Jenista Mhagama akiwa anamsikiliza Balozi wa Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro Mrisho Mpoto mara baada ya kuwasili katika banda hilo hivi karibuni jijini Arusha katika maadhimisho ya sikukuu ya nane nane


Ofisa Utalii wa Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro Peter Makutian aliwashukuru watanzania kuendelea kuhamasika kutembelea hifadhi hiyo tofauti na awali na kusema kuwa idadi ya wageni toka nje ya nchi wanaotembelea hifadhi hiyo kwasasa ipo sawa na watanzania.
Na Pamela Mollel,Arusha

WAZIRI wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Jenista Mhagama amezitaka hifadhi za taifa nchini kuendelea kuwatumia wasanii nchini katika kutangaza vivutio mbalimbali vinavyopatikana huku akiipongeza Mamlaka ya hifadhi za taifa Ngorongoro inavyotangaza vivutio vyake kupitia msanii Mrisho Mpoto.


Kauli hiyo aliitoa hivi karibuni  jijini Arusha alipotembelea banda la Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro katika maonesho ya Nanenane.

Alisema kuwa wasanii wananafasi kubwa ya kuutangaza utalii wa ndani na kuendelea kuitangaza Tanzania endapo watatumiwa kama mabalozi kupitia umaarufu wao jambo ambalo litasaidia pia kuiingizia nchi kipato kupitia watalii.

Naye Balozi wa Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro Mrisho Mpoto aliwapongeza watanzania kuwa na mwitikio mkubwa wa kutembelea hifadhi hiyo ikiwa ni pamoja na kuwapeleka watoto wao katika maonesho hayo ili kujifunza na kuona shughuli zinazofanywa na mamlaka hiyo hivyo kuwaandaa watoto hao kuwa wahifadhi kwa baadae.

"Mfano mzuri ni hili la punguzo la shilingi elfu 50 lililotolewa ili watanzania waweze kutembelea hifadhi ya Ngorongoro tumeona watu walivyochangamkia na kwenda kutembelea Ngorongoro  hivyo ni jambo zuri na la kupongezwa kwa watanzania  na ninaomba waendelee kutembelea hifadhi zetu"alisema Mpoto.

Kwa upande wake Ofisa Utalii wa Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro Peter Makutian aliwashukuru watanzania kuendelea kuhamasika kutembelea hifadhi hiyo tofauti na awali na kusema kuwa idadi ya wageni toka nje ya nchi wanaotembelea hifadhi hiyo kwasasa ipo sawa na watanzania.

Aidha aliwaomba watanzania wengine kuendelea kutembelea vivutio vya Tanzania ikiwemo Ngorongoro kwakuwa gharama wanazotoza ni ndogo kwao ukilinganisha na wageni toka nje ya nchi hivyo ni fursa nzuri kwao kuitumia na kuwa mabalozi wa hifadhi kwa wengine.

DK. KIGWANGALLA AANZA ZIARA YA KIKAZI ARUSHA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
Naibu Waziri wa Afya, Maemdeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (MB), akitoa maelezo kwa uongozi wa Kituo cha Afya Kaloleni namna watakavyojenga wodi ya Wazazi katika moja ya maeneo ndani ya kituo hicho cha Afya Kaloleni, Wilaya ya Arusha, mapema leo Agosti 17,2017 wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea vituo mbalimbali vya Afya na kujionea utendaji kazi katika sekta hiyo ya Afya Mkoani hapa.

Naibu Waziri wa Afya, Maemdeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (MB), akitoa maelezo kwa uongozi wa kituo cha Afya Levolosi juu ya uwekaji wa vifaa vya Maabara hiyo

Dk. Kigwangalla akkagua chumba cha upasuaji katika kituo cha Afya Levolosi

Dk. Kigwangalla akikatisha mitaa kwa miguu akitokea kituo cha Afya Levolosi wakati akielekea kukagua kituo cha Afya cha Ngarenaro

Dk. Kigwangalla akikatisha mitaa kwa miguu akitokea kituo cha Afya Levolosi wakati akielekea kukagua kituo cha Afya cha Ngarenaro

Dk. Kigwangalla akikatisha mitaa kwa miguu akitokea kituo cha Afya Levolosi wakati akielekea kukagua kituo cha Afya cha Ngarenaro. Kulia kwake ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dk. V. Timothi Wonanji na kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya jiji la Arusha Dk. Baraka Mundhe.

Dk. Kigwangalla akikagua kituo cha Afya ambacho kinajengwa cha Muriet Mpya wakati wa ziara yake hiyo.

Dk. Kigwangalla akikagua kituo cha Afya ambacho kinajengwa cha Muriet Mpya wakati wa ziara yake hiyo.

Dk. Kigwangalla akiwa katika kituo cha Afya Themi wakati wa ziara yake hiyo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Rebecca Mongi

Dk. Kigwangalla akikagua kituo cha Afya kinachojengwa wakati wa ziara yake hiyo.

Dk. Kigwangalla akipata picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa sekta ya Afya Jiji la Arusha wakati wa ziara yake hiyo.

Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya jiji la Arusha Dk. Baraka Mundhe akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla wakati alipotembelea kituo cha Afya Kaloleni.

Dk. Kigwangalla akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati akizungumza na waandishi wa habari

Dk. Kigwangalla akitoa maagizo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Bi. Rebecca Mongi wakati wa ziara yake hiyo ya kukagua vituo vya Afya

DR.DALLO OLE WAKE MGOMBEA ATAKAE ENDA KINYUME NA SHERIA YA UCHAGUZI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Na Woinde Shizza,ArushaWagombea wa nafasi mbalimbali za ungozi ndani ya chama cha mapinduzi wilaya wa Arusha wametakiwa kufuata kanuni na sheria za zilizowekwa  na chama hicho.Hayo yamebainishwa na katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Arusha Dr, Ramathani Dallo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na  tuhuma za kuwepo na baadhi ya wagombea kuja kwenye usahili na watu wanaodaiwa sio wagombea bali ni waganga wa kienyejiAlisema kuwa ni muhimu sana wagombea wakifuata kanuni taratibu na sheria zilizowekwa  katika uchaguzi  kwa mujibu wa kanuni ya  muongozo wa uchaguzi ya mwaka 2010Alisema kuwa yeye binafsi ajawaoana watu hao wanaodaiwa ni waganga wa kienyeji na usahili  ulienda vizuri na k atika kipindi hichi  uchaguzi unaendelea vyema ,huku akibainisha kuwa iwapo kutakuwa na mgombea yeyote ambae atakwenda kinyume na sheria ya uchaguzi atamuaonea huruma bali atuakali zidi yake itachukuliwa .“nasema kwakweli ili swala na mgombea  wa UWT kuja na mganga wa kienyeji kwenye usaili sijaliona ila ukweli napenda kuchukua nafasi hiii kuwasihi iwapo tutamkamata mgombea yeyote Yule anaekwenda kinyume na sheria tutamchukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuinta kikao kama jambo ni gumu sana pia itatulazimu tumkate jina lake na asiwepo kwenye kinyanganyiro chochote”alisema Dr,Dallo

Alizitaja baadhi yakanuni kuwa ni pamoja na kutofanya kampeni ,kukusanya watu kufanya mikutano isioyo rasmi kichama pamoja na  nyingi Aidha akiongelea baadhi za uchaguzi zilizopita alisema kwa upande wa uchaguzi wa kata ,mitaaa umemalizika vizuri sasa ivi ndio wanaendelea na maeneo mengine yaliyobakiAwali baadhi ya wagombea ambao hawakutaka majina yao yaandikwe walisema kuwa kuna mmoja wa mgombea mwenza sik u ya usahili alikuja akiwa na mganga wa kienyeji kitu ambacho ni kinyume na sheria ya uchaguzi

TAARIFA KWA UMMA JUU YA ZOEZI LA KUONDOA MIFUGO NA MAKAZI NDANI YA HIFADHI YA TAIFA SERENGETI NA KWENYE MPAKA WA PORI TENGEFU LOLIONDO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

TAARIFA KWA UMMA

ZOEZI LA KUONDOA MIFUGO NA MAKAZI NDANI YA HIFADHI YA TAIFA SERENGETI NA KWENYE MPAKA WA PORI TENGEFU LOLIONDO

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ngorongoro, kwa kushirikisha Hifadhi ya Taifa Serengeti na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, inaendesha zoezi la kuondoa mifugo na makazi ndani ya hifadhi ya Taifa Serengeti na kwenye mpaka wa Pori Tengefu Loliondo.

Zoezi hilo lililoanza tarehe 10  Agosti 2017  litadumu kwa siku kumi na nne na linashirikisha Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ngorongoro, Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Hifadhi ya Taifa Serengeti na Hifadhi ya eneo la Ngorongoro.

Zoezi hilo linalenga kunusuru uhifadhi ndani ya hifadhi, ndani ya Pori Tengefu Loliondo, na ndani ya mfumo ikolojia wa Serengeti na pia kunusuru utalii katika mfumo ikolojia huo.

Aidha, hatua hii ya kuondoa makazi na mifugo kutoka katika maeneo ya mipaka ya Pori Tengefu Loliondo kutaongeza uhakika wa kupatikana malisho ya mifugo wakati wa kiangazi kwa kuwa hakutakuwepo na makazi ndani ya Hifadhi na ufugaji holela.

kimsingi zoezi hili linaendana na wito wa Serikali wa kuondoa mifugo ndani ya maeneo yote yaliyohifadhiwa nchini.

Katika kutekeleza zoezi hili, Mkuu wa Wilaya  Ngorongoro, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ngorongoro Bwana Rashidi Taka, alitoa maelekezo yafuatayo:

1. Zoezi litafanyika ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti na kwenye mpaka wa Pori Tengefu Loliondo. Kwa upande wa mpaka wa Pori Tengefu Loliondo zoezi litaanzia kaskazini hadi kusini urefu wa kilometa 90, na upana wake utakuwa kilometa 5. Kwa ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti litafanyika upande wa mashariki kuanzia milima ya Kuka (kaskazini) hadi kigingi na. SNP 9 (kusini); 

2. Maboma yatakayokutwa ndani ya hifadhi yatateketezwa kwa moto na watu watakaokutwa na mifugo watachukuliwa hatua za kisheria, ikiwemo kupelekwa mahakamani;

3.  Maboma yaliyoko ndani ya mpaka wa Pori Tengefu Loliondo -  kwenye mpaka na ndani ya kilometa tano - wataondolewa ili warudi vijijini. Eneo hilo litabaki kwa ajili ya malisho na si kwa ajili ya makazi.  Uwepo wa makazi kwenye mpaka wa Hifadhi ya Taifa Serengeti umekuwa kichocheo kikubwa cha mifugo kuingizwa hifadhini.

Zoezi hili linalenga kuondoa changamoto kubwa ya mifugo kuingizwa Hifadhi ya Taifa Serengeti na kwenye mpaka wa Pori Tengefu Loliondo, kupambana na uvamizi mkubwa uliofanywa na wahamiaji haramu kutoka nchi jirani na kunusuru vyanzo vya maji kutokana na mifugo kulishwa kwenye vyanzo vya maji na hivyo kusababisha vyanzo hivyo kuharibika na kukosekana kwa maji kwa ajili ya mifugo na wanyamapori.

Hadi sasa zoezi hili la kuondoa mifugo na makazi ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti na kwenye mpaka wa Pori Tengefu Loliondo linaendelea vizuri likihusisha kuchoma moto maboma yote yaliyoachwa na wafugaji walioondoka wakati wa zoezi.

Wizara ya Maliasili na Utalii inapenda kuufahamisha umma kuwa hakuna watu wanaopigwa katika zoezi hili.

Pia, Wizara ya Maliasili na Utalii inapenda kuutaarifu umma kuwa habari zinazosambazwa mitandaoni ni upotoshaji wa ukweli wenye nia ovu ya kujenga chuki dhidi ya Serikali  kwa wananchi wa Loliondo na maeneo yanayopitiwa na zoezi hilo.

Aidha, Wizara ya Maliasili na Utalii, inapenda kuweka bayana kuwa, taarifa za kupigwa risasi Pormoson Losso mwenye umri wa miaka 23, mkazi wa Ololosokwan zilitolewa tarehe 8 Agosti 2017 na hazihusiani na zoezi tajwa kwani tukio hilo  lilitokea siku tano kabla ya kuanza zoezi la kuondoa mifugo na makazi ndani ya hifadhi wakati zoezi hili lilianza kutekelezwa Jumapili tarehe 13 Agosti 2017.

Hata hivyo Serikali inawapongeza wananchi wengi miongoni mwa wafugaji kwa kuunga mkono zoezi hili na kwa ushirikiano wanaotoa.
Serikali inatoa onyo kwa yeyote anayejihusisha na upotoshaji wa ukweli kuhusu zoezi hili lenye nia njema linalolenga kunusuru hifadhi, kuacha mara moja ili kujiepusha na hatua za kisheria zitakazochukuliwa pindi atakapobainika.

Imetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

17/08/2017
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa